ATTENTION: This is how you lose weight!

ATTENTION: This is how you lose weight!

Unataka kupunguza uzito na ujui cha kufanya ili kuondokana na tatizo hilo, basi soma dondoo hii maalum ambayo MwananchiScoop imekuandalia.

 

Tatizo la uzito mkubwa wa mwili linawakumbwa wengi lakini leo tumekuletea vyakula ambavyo mtu akiwa anakula na kufanya mazoezi basi anaweza kupungua uzito.

 

Mboga za majani

 

Moja ya vyakula hivyo ni ulaji wa mboga za majani kwa wingi. Hapa tunazungumzia mchicha, matembele, kisamvu, mnafu, sukuma wiki, nyanya chungu, bamia na nyengine nyingi.

 

Mboga hizi zimebeba vitamin na wanga kidogo hivyo zinaweza kuliwa kwa wingi bila ya kujaza tumbo hivyo hazisababishi unene.

 

Mayai

 

Pia mayai yana protini nyingi sana ambazo zinamtosha kifaranga kutoka ndani ya yai hilo akiwa mzima, utafiti unaonyesha binadamu wa kawaida anatakiwa awe anakula mayai angalau matatu kwa siku kuondoa uwezekano wa kupata cholestro ambazo ni hatari kwa moyo.

 

Mayai yanayozungumziwa hapa ni mayai ya kienyeji, ukiwa unakula mayai asubuhi kama sehemu ya kifungua kinywa chako utakaa muda mrefu bila njaa.

 

Samaki

 

Samaki jamani pia ni miongoni chakula ambavyo ukila vitakufanya uweze kupungua uzito.

 

Fahamu kuwa samaki wana kiasi kidogo cha mafuta, wana protini ambayo itakuacha muda mrefu ukiwa umeshiba na kukufanya usile sana, lakini pia samaki wanakemikali ya Omega 3 ambayo ni muhimu sana kwenye mwili huzuia magonjwa na kusaidia kazi ya kuchoma mafuta.

 

Maparachichi

 

Parachichi ni moja kati ya tunda ambalo linamafuta na nyuzi ambazo ni muhimu sana kwa afya na moyo pamoja na kupunguza uzito.

 

Maparachichi yanamafuta aina ya oleic oil ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya mizaituni au olive oil na hua yanamfanya mlaji kutoishiwa maji mwilini.

 

Viazi mviringo vya kuchemsha

 

Viazi mviringo ni moja ya chakula kizuri ambacho kinaweza  kupunguza uzito wa mwili.

 

Viazi hizi vina sukari kidogo na kiasi kikubwa cha potassium, japo watu wengi hupenda zaidi kuvikaanga na kuvila kama chipsi.

 

Mazingatio, hivyo ni baadhi tu ya vyakula vya kupunguza uzito lakini unaweza pia kutumia na vyakula hivi ikiwemo nyama ya kuku, karanga na korosho, maharage, mafuta ya maji pamoja na maziwa.






Comments 2


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags