Atengwa na jamii baada ya kupoteza watoto saba

Atengwa na jamii baada ya kupoteza watoto saba

Mwanamke mmoja nchini Kenya aliye fahamika kwa jina la Margaret Wamaitha atengwa na jamii baada kuwapoteza watoto wake sita na kubeba ujauzito mara saba bila kupata mtoto katika mazingira ya kutatanisha.

Mama huyo alifanikiwa kupata mtoto mmoja pekee huku akiwapoteza wengine kwa njia ya upasuaji alisema wengi walidai kuwa alilaaniwa, huku wengine wakisema aliwatoa watoto wake kafara.

“Watu walisema nimelaaniwa wengine waliniambia nifate wazee na mbuzi ili wamchinje na kunisafisha” alisema Margaret.

Aliongeza kwa kusema baadhi ya watu walimshauri vibaya kwenda kwa waganga ambao wangeweza kumsaidia katika hali yake kutokana na kukataliwa na jamii na kupigwa vita kanisani.

“Wachungaji wanatumia hadithi yangu wakidai nilikuwa mkaidi, ndiyo maana Mungu alikuwa akichukua watoto wangu wengine walithubutu kuniambia ninawatoa watoto wangu kafara” alisema huku machozi yakitiririka mashavuni mwake.

Hali hiyo imemfanya awe mwenye kukata tamaa kwa makosa mbayo yeye mwenye imekuwa ni kitendawili kuyajua.

Chanzo TUKO






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags