Aslay arudi mjini kwa kishindo

Aslay arudi mjini kwa kishindo

Aloooooh! Unaambiwa mambo yametaradadi sio powa yani, baada ya ukimya wa muda mrefu yule msanii mkongwe aliependwa na anaezidi kupendwa  na kila mja Aslay amefunguka na kusema kuwa mashabiki zake wategemee makubwa sana kutoka kwake.

Aslay ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa “Ninafuraha kuwaambia Mashabiki, Vyombo vya habari na kila anayenifuatilia kwamba hivi karibuni nimejiunga na RockStar Africa
Imekuwa safari ndefu yenye matumaini makubwa katika kusimamia kazi zangu za muziki” ameendelea kwa kuandika kuwa


“Hivyo basi, Nawaarifu kutegemea mengi makubwa katika muziki wangu na kuniona katika hatua kubwa zaidi. Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi chote ambacho nilikuwa kimya, hakika nimejifunza Mengi. Ningependa kuchukua wakati huu Pia kutoa shukrani zangu kwa kila mmoja wenu kwa support mnayoendelea kunipa katika muziki wangu hata wakati nilipokuwa kimya niseme tu Asanteni sana” ameandika Aslay

Wooooyooo! Haya haya wale wadau wa Aslay haya mwenenu anarudi mjini kwa kishindo, una jambo gani la kumueleza msanii huyu dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags