Askali wapewa saa 24 kukamatwa

Askali wapewa saa 24 kukamatwa

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa saa 24 kwa Jeshi la Polisi kuwakamata askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wanaotuhumiwa kuwapiga, kuwajeruhi, kuwadhalilisha wananchi pamoja na kupora mifugo yao huko Mbarali.

 “Nimetoa maagizo kwa kamanda wa Polisi wa Mkoa ahakikishe wale askari wote waliofanya kitendo kama hicho, wakamatwe, wapelekwe polisi na wafunguliwe kesi kama raia wengine” ameagiza hayo Homera.

Homera ametoa agizo hilo mara baada ya kukutana na kuzungumza na wananchi ambao wamelalamikia vitendo hivyo vya uvunjifu wa sheria, akisisitiza kuwa serikali haiwatumi askari kuwapiga wananchi wasio kuwa na hatia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags