Arteta amkingia kifua Raya

Arteta amkingia kifua Raya

‘Kocha’ wa ‘klabu’ ya #Arsenal, Mikel Arteta amtetea ‘goli kipa’ wa ‘timu’ hiyo David Raya baada ya mchambuzi wa ‘timu’ hiyo Gary Neville kudai kuwa kiwango cha sasa cha ‘kipa’ huyo kitawagharimu katika mipango yao ya kubeba ubingwa msimu huu.

Raya hivi karibuni amekuwa akifanya makosa ya kiufundi hasa katika ‘mechi’ iliyochezwa weekend iliyopita kwa kuiruhusu ‘klabu’ ya #Chelsea kufunga kupitia #MykhayloMudryk.

Baada ya ‘mechi’ hiyo kuisha Neville alizungumza wasiwasi wake juu ya ‘kipa’ huyo kwa kudai hana uwezo wa kumudu presha ya kuchezea ‘timu’ kubwa na huenda ikawagharimu katika kuchukua ubingwa.

Lakini ‘kocha’Arteta ameeleza kuwa hajaona makosa makubwa kwa ‘kipa’ huyo na hana wasiwasi naye anajua ni kawaida kukosa mchezo na mara zote anaona ‘kipa’ huyo anacheza katika kiwango cha juu kama ilivyo kawaida yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags