Arsenal, Man United zapigana vikumbo kwa Brahim Diaz

Arsenal, Man United zapigana vikumbo kwa Brahim Diaz

Imefahamika kuwa ‘klabu’ za Arsenal na Manchester United zipo katika vita kali ya kumwania mshambuliaji wa mabingwa wa ‘soka’ nchini Hispania, Real Madrid, Brahim Abdelkader Díaz.

Taarifa zinaeleza kuwa, Brahim anajiandaa kuondoka Real Madrid, kufuatia usajiliwa wa mshambuliaji kutoka Ufaransa, Kilyan Mbappe.

Usajili wa Mbappe unatajwa kama kizingiti kwa Brahim kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao Barani Ulaya.

Kwa muda mrefu Arsenal ilikua katika mpango wa kumsajili Brahim na iliaminika huenda ingekuwa ‘klabu’ pekee katika harakati hizo, lakini kuingia kwa Man United kunafungua ukurasa mpya wa ushindani wa kuiwania saini ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

Kwa sasa ada ya usajili ya Brahim, ambaye alikuzwa na kuendelezwa kisoka na mabingwa wa soka nchini England, Manchester City inatajwa kufikia Euro 70 milioni. Hata hivyo, bado ana mkataba na Real Madrid hadi 2027.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags