Arnold Schwarzenegger aendelea kula chumvi

Arnold Schwarzenegger aendelea kula chumvi

Tarehe kama ya leo Julai 30, 1947 alizaliwa mwigizaji mkongwe kutoka Marekani, Arnold Schwarzenegger ambaye sasa ametimiza miaka 77.

Mkali huyo wa Filamu ya ‘Terminator’ alizaliwa katika Jimbo la Thal nchini Austria ambapo mpaka kufikia sasa ametajwa kuigiza zaidi ya filamu 40 huku ile ya kwanza ikiwa ni ‘Hercules in New York’ iliyotoka mwaka 1970.

Schwarzenegger ‘Komando Kipensi’ ameonekana katika filamu kama ‘The Terminator’, ‘Predator’, ‘Commando’, ‘The Running Man’ ‘Aftermath’, ‘The 6th Day’ na nyinginezo.

Mbali na kuupiga mwingi katika uigizaji pia aliwahi kuondoka na mataji kadhaa katika mchezo wa kutunisha misuli ikiwemo ushindi mara tano wa Mr. Universe (4 – NABBA England], 1 – IFBB [USA]), na ushindi mara saba wa ‘Mr Olympia’.

Katika taaluma iliyomleta mjini ya uigizaji amewahi kuchukua tuzo kama Tuzo za Filamu za 1991 MTV-Mwigizaji Bora, 1995 Golden Globe katika kipengele cha ‘Best Performance by an Actor in a Motion Picture - Musical or Comedy’ na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags