Apokea maua ya valentine kutoka kwa marehemu mumewe

Apokea maua ya valentine kutoka kwa marehemu mumewe


Kuna msemo usemao mapenzi ya kweli hayajifichi, msemo huu unajidhihirisha kwa mwanamama Diana Maver, (77) ambaye anaendelea kupokea zawadi za maua katika siku ya Valentine kutoka kwa marehemu mumewe.

Inaweza kuwa inashangaza kuona mtu anapokea zawadi kutoka kwa marehemu lakini kwa mume wa Diana Maver, Bwana John Maver enzi za uhai wake aliamua kumlipa muuzaji maua ili aweze kuwa anampelekea zawadi hiyo mkewe kila ifikapo Februari 14, siku ya Wapendanao ‘Valentines Day’, kwa maisha yake yote.

John Maver na Diana Maver, walianza mahusiano tangu wakiwa na miaka 16, mpaka walipofunga ndoa miaka 47 iliyopita ambapo mumewe huyo alifariki Oktoba 2017, na toka mwaka huo Diana amekuwa akipokea zawadi za maua kwa miaka 7 mpaka kufikia sasa.

Mtoto wa Diana, Heard Maver, alifunguka kupitia tovuti ya ‘ABC San Francisco station KGO’ na kueleza kuwa baba yake alikuwa na upendo wa dhati kwa mama yake, hivyo anaamini upendo unaweza kuwepo katika maisha ya kawaida na kifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags