Apigwa faini baada ya kamera kumnasa akijikuna shavu

Apigwa faini baada ya kamera kumnasa akijikuna shavu

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Liu kutoka nchini China amepigwa faini baada ya kamera za barabarani kumnasa akijikuna shavu.

Kulingana na gazeti la Jilu Evening Post, linaeleza kuwa dereva huyo alikuwa akiendesha gari Jumatatu katika mji wa Jinan, mashariki mwa jimbo la Shandong, na alinyanyua mkono wake kujikuna usoni alipokuwa akipita mbele ya kamera inayotumia akili bandia.

Kwa mujibu wa maelezo aliyoyapokea kutoka mamlaka ya trafiki jijini humo ilimtaarifu kuwa alikuwa amekiuka sheria za barabarani kwa kuendesha gari huku akiongea na simu, hivyo anatakiwa kulipa faini ya dola 7.25 ikiwa ni zaidi ya Elfu 19 za Kitanzania.

Aidha mwanaume huyo wakati akiwa kwenye mahojiano yake na Microblog aliweka wazi kuwa haitambui faini hiyo huku akiita ni ya kipuuzi kwani kumekuwa na matukio mabaya barabarani yanayosambazwa mitandaoni yakivunja sheria za barabarari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags