Aomba talaka akidai mumewe mchafu

Aomba talaka akidai mumewe mchafu

Mwanamke mmoja kutoka nchini #Uturuki aliyejitambulisha kwa jina la #AY ameripotiwa kuomba talaka akidai kuwa mumewe aitwaye #CY hakuwa msafi wa mwili.

#AY alifikisha ombi la talaka Mahakamani pamoja na mashaidi ambao walithibitisha kuwa mume wa #AY ni mchafu hakuwa akioga wala kupiga mswaki.

Kulingana chombo cha habari kutoka #Uturuki cha ‘#Sabah’ kilieleza kuwa #Mahakama ya 19 ya Familia ilimkuta na makosa mwanaume huyo ambayo yasingeweza kuvumilika kwenye ndoa ndipo ikabidi AY kupewa talaka yake na fidia ya dola 16,419.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags