Angelique atoa neno kwa wasanii wanaoimba kusifia siasa

Angelique atoa neno kwa wasanii wanaoimba kusifia siasa

Glorian Sulle

Mwanamuziki Angelique Kidjo (64) raia wa Benin amewataka wasanii ambao ni kama kioo cha jamii kutoa maoni kuhusu siasa na si kusifia chama.

Kidjo amesema endapo msanii atakuwa na kazi ya kusifia chama ni rahisi kupotea kwenye muziki lakini akiitumia sanaa yake kwa kutoa maoni basi itamfanya adumu na kuona faida katika muziki.

Akiwa katika moja ya mahojiano na kituo cha Television cha Al Jazeera, amesema kwa upande wake alishauriwa na baba yake kutojihusisha na siasa kwa kuimba wimbo wowote wa kusifia chama.

"Baba yangu amekuwa akinishauri kutotunga nyimbo za kusifu vyama vya siasa kwani vinakuja na kuondoka,” amesema.

Licha ya uimbaji wake wa tofauti, Kidjo pia ni mwigizaji aliyetamba miaka ya 2022 na hata kufahamika zaidi kupitia filamu ya The Woman King (the Meunon) akibeba majukumu ya kiongozi katika jamii hiyo.

Mbali na uigizaji na uimbaji, Kidjo ni mke halali wa mwanamuziki na mtayarishaji wa nyimbo kutoka Ufaransa, Jean Hebrail, katika ndoa ya wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja wa kike Naima Hebrail ambaye ni mwigizaji na mwandishi wa wimbo.

Mbali na tuzo tano za Grammy, Kidjo mpaka sasa ana albamu 16 huku akitamba na kibao chake kipya alichokipa jina la “Joy” akimshirikisha mwanamuziki kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke (Davido).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post