Amuua Mtoto akidhani Ng’ombe Njombe

Amuua Mtoto akidhani Ng’ombe Njombe

Hii imetokea huko mkoani Njombe baada ya Jeshi la Polisi Mkoani humo wa linamshikilia Mwanamke mmoja aitwaye Estaroda Kaduma (28) amkazi wa Kichiwa kwa tuhuma za kumuua Mtoto wa Kaka yake anayefahamika kwa jina la Brown James Kaduma (7) ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kichiwa.

Akizungumzia tukio hilo jinsi lilivyotokea Kamanda wa Polisi mkoani humo Hamis Issah amesema Kijana huyo alikuwa amelala majira ya saa nane usiku wakati Shangazi yake akiwa anafanya maombi lakini cha kushangaza alianza kupambana kwa kumpiga Mtoto akidhani ni ng’ombe mkubwa mweusi aliyefika wakati akifanya maombi.

“Huyu Dada huwa ana tabia ya kufanya maombi na katika maombi yake akaona ng’ombe mkubwa mweusi amefika katika eneo ambalo anafanya maombi, akaacha maombi akaanza kumpiga huyo ng’ombe na baadaye akatoweka baada ya muda akaonekana amefariki Kijana mdogo Mtoto wa Kaka yake baada ya kukanyagwakanyagwa kichwani na kujeruhiwa sehemu nyingine za mwili”

Hata hivyo Kamanda Issah amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina na kutoa wito kwa Wananchi kuachana na imani hizo ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa kwenye jamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags