Amshitaki ‘Ex’ wake kwa kutomsindikiza uwanja wa ndege

Amshitaki ‘Ex’ wake kwa kutomsindikiza uwanja wa ndege

Mwanamke mmoja kutoka New Zealand, aliyetambulika kwa jina la CL amemshitaki mpenzi wake wa zamani kwa kushindwa kumpeleka (kumsindikiza) uwanja wa ndege wakati wa kusafiri.

Kwa mujibu wa ‘Sky News’ imeeleza kuwa kulingana na madai hayo yaliyofikishwa mahakamani yanaeleza kuwa wawili hao walifanya makubaliano ya mdomo kwamba mwanaume huyo angempeleka uwanja wa ndege wakati ya safari yake ya kurudi nyumbani kwao pamoja na kutunza mbwa wake.

Hata hivyo kwa mujibu wa hati hizo mwanadada huyo alieleza kuwa baada ya mpenzi wake kutompeleka uwanja wa ndege alichelewa ndege yake na kumgharimu kununua tiketi nyingine hivyo amefungua kesi hiyo kwa ajili ya kudai fidia ya dola 27,000.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika Mahakama ya Mizozo ya New Zealand, ambayo inashughulikia na madai madogo, ilitupilia mbali kesi hiyo ikieleza kuwa ahadi za ndugu au marafiki zinaweza kuvunjika muda wowote kwani haziwekwi kisheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags