Aliyezikwa hai siku saba akiandaa maudhui, Aibuka na tukio jingine

Aliyezikwa hai siku saba akiandaa maudhui, Aibuka na tukio jingine

Muandaaji maudhui kwenye mtandao wa #YouTube kutoka nchini Marekani Mr Beast baada ya video yake akiwa amezikwa hai kwa siku 7 kufanya vizuri kwenye mtandao YouTube, sasa amefanya challange nyingine ya kuwaweka watu wawili wasiofahamiana kwenye chumba kimoja ndani ya siku mia moja.

Watu hao wawili akiwa mwanamke mmoja aitwaye Suzie na mwanaume mmoja aitwaye Bailey walilazimika kuishi kwenye chumba kimoja ndani ya siku 100 kwa kufata sheria ya chumba hicho ili waweze kushinda dola 500,000 ambazo ni zaidi ya Sh1.2 bilioni.

Kati ya sheria walizokuwa wamewekewa ni kukaa mbali na simu zao ndani ya siku zote hizo, kutokuwa na kitu chochote cha kuwaburudisha katika chumba hicho, kutokana na kutovunja sheria hizo wawili hao wamefaniki kuondoka na kitita hicho.

Hadi sasa video ya wawili hao wakiwa katika chumba hicho ina watazamaji zaidi ya milioni 57. Hii si mara ya kwanza kwa mwanamitandao huyo kupata watazamaji wengi kwenye mtandao wake wa YouTube mwezi mmoja uliopita, aliandaa maudhui ya kuzikwa hai ndani ya siku saba akiwa live kwenye kaburi lililokuwa na matobo ya kuingiza hewa na kisha kujipatia watazamaji milioni 113 kwenye mtandao huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags