Aliyetuhumiwa kumuua mwalimu mwenzake naye adaiwa kujiua

Aliyetuhumiwa kumuua mwalimu mwenzake naye adaiwa kujiua

Mwalimu Samuel Subi wa shule ya msingi Igaka, anayetuhumiwa kumuua mwalimu mwenzake kisa uongozi, amekutwa amejinyonga kwa kutumia shati alilovaa akiwa mahabusu Machi 17, 2022.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amesema “Subi aliingia chooni na kutumia shati lake kujinyonga, mahabusu wenzake waligundua dakika za mwisho na kumsaidia, alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa kwa matibabu lakini alifariki dunia”

Mwalimu Subi alituhumiwa kumuua Emmanuel Chacha kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya moyo, chanzo kikitajwa kuwa ni kugombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags