Aliyetaka kumteka mtoto wa Neymar akamatwa

Aliyetaka kumteka mtoto wa Neymar akamatwa

Kijana wa miaka 20 anashikiliwa na polisi baada ya jaribio la kutaka kumteka mtoto wa kike wa mchezaji kutoka ‘Klabu’ ya Al Hilal, #Neymar baada ya kuvamia nyumba ya mpenzi wa mchezaji huyo Bruno Bianrcadi nchini #Brazil.

Tukio hilo limetokea jana Jumanne Novemba 7 ambapo watu watatu waliodaiwa kuwa na silaha walivamia nyumba ya #Bianrcadi kwa lengo la kumteka mrembo huyo na mtoto wake #Mavie, lakini walishindwa kuwapata kutokana na wawili hao kutokuwepo nyumbani.

Aidha polisi walifika eneo la tukio na kukuta wazazi wa #Biancardi wakiwa wamefungwa na kuzibwa midomo katika nyumba hiyo ambapo mmoja wa majambazi hao alikamatwa na polisi huku wengine wawili walifanikiwa kukimbia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags