Aliyepigwa na Mike Tyson adai fidia

Aliyepigwa na Mike Tyson adai fidia

Mwanamume mmoja kutoka nchini Marekani aitwaye Melvin Townsend ambaye alipokea kichapo kutoka mkali wa ngumu Mike Tyson ndani ya ndege, amefunguma mashitaka ya kudai fidia ya dola 450k ambazo ni sawa na tsh bilioni 1.1.

Melvin amedai kuwa ngumi alizopigwa na Tyson zilimsababishia maumivu makali ya kichwa hivyo anadai fidia aliyotumia katika matibabu, huku mwanasheria wa Tyson amesema kuwa hakuna malipo yoyote yatakayolipwa kufuatiwa na tukio hilo.

Ikumbukwe kuwa tukio hilo lilitokea April 2022 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa San Francisco, baada ya Melvin kumchokoza na kumtolea maneno machafu Mike Tyson.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags