Aliyempata mbwa wa Lady Gaga aambulia patupu

Aliyempata mbwa wa Lady Gaga aambulia patupu

Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Lady Gaga hatoruhusiwa tena kumlipa mwanamke ambaye alirudisha mbwa wake baada ya kuibiwa mwaka 2021 ambapo pesa hiyo aliahidi kama zawadi.

Kufuatia uamuzi wa mahakama ya Los Angeles uliofanyika Jumatatu ya wiki hii kuwa Gaga hakutakiwa kumlipa mwanamama Jennifer McBride, baada ya kugundulika kuwa alimteka mbwa huyo.

Jennifer alimshitaki Lady Gaga kwa kutosema wala kumlipa chochote baada ya kutangaza kuwa atakayempata mbwa wake atampa zawadi ya zaidi ya dola 500,000 pamoja na fidia ya $1.5m, mwanamama huyo alifungua ‘kesi’ ya ulaghai na ahadi za uongo.

Lakini hakimu alisema kuwa McBride hatakiwi kudai pesa hizo kwa sababu hatua ya kurudisha mbwa wa nyota huyo ilisababisha kukutwa na makosa ya kupokea bidhaa zinazoibwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags