Alikiba kama Diamond tu

Alikiba kama Diamond tu

Usiku wa kuamkia leo Februari 27,2025 kulikuwa na tamasha kubwa ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza

Katika tuzo hizo ambazo, zilifanyika Zanzibar Kisiwani Unguja mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba aliondoka bila kutumbuiza. Tukio hilo ambalo limezua mijadala kwa baadhi ya wadau wa muziki huku wakiwepo wanaomponda na wanaopongeza.

Kati ya sababu za msanii huyo kuondoka bila kutumbuiza zinatajwa ni kutokuwa na mazingira rafiki ya tamasha hilo. Hata hivyo, hii inakuwa siyo mara ya kwanza kwa msanii kuondoka kwenye tamasha bila kuruka na mashabiki wake.

Utakumbuka mwishoni mwa mwaka 2024, mwanamuziki Diamond hakuweza kutumbuiza katika Tamasha la Furaha City lililofanyika nchini Kenya. Licha ya kuwepo eneo la tukio baada ya kuzuka vurugu katika eneo hilo.

“Siwezi kuja kwenye event (tukio) halafu nika-force (lazimisha) nipande kwenye stage (jukwaa), wewe umeshanilipa, mimi nasubiri muda wangu wa kuperfom (kutumbuiza), nikiona muda huu siyo wa kupanda kwenye stage (jukwaa) naondoka zangu. Siwezi ku-force, ukishindwa kunipandisha katika muda tuliokubaliana naondoka zangu na pesa yako nakuwa nimeila,” alieleza Diamond baada ya kuondoka kwenye tamasha hilo.

Hivyo basi tukio hilo la Alikiba linakumbusha mashabiki mkasa wa Diamond nchini Kenya ambako alisubiriwa kwa hamu. Aidha siyo hao tuu pia wapo mastaa wengine ambao waliwahi kuondoka kwenye show bila kutumbuiza akiwemo Burna Boy kwenye show yake ya Lagos, Nigeria mwaka 2023. Vilevile Wizkid aliwahi kuondoka kwenye onyesho nchini Ivory Coast mwaka 2022 .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags