Alikiba afunguka mipango ya kuupeleka muziki wake Kimataifa

Alikiba afunguka mipango ya kuupeleka muziki wake Kimataifa

Mwanamuziki Ali Saleh Kiba, maarufu Alikiba amefunguka kuhusiana na plani zake za kuupeleka muziki wake Kimataifa kama wasanii wengine kwa kuweka wazi kuwa anamipango wa kufanya hivyo lakini anaamini wakati wake bado.

Nyota huyo anayetamba na ngoma kama ‘Huku’ na ‘Sumu’ alifunguka hayo wakati wa uzinduzi wa runinga yake ya ‘Crown TV’ usiku wa kuamkiaa leo Septemba 14 huku akidai kuwa kila msanii anaplani zake hivyo basi kwa upande wake anaona sio wakati wake.

“International it’s a matter of time, kila msanii anakuwa na strategies zake, ikifikia wakati mtatuona tu mambo yakikaa sawa mtatuona huko, plan yangu ilikuwa ni international album, kwa sababu haijawa tayari na haijakamilika, nimeona niwape EP, watu waendelee kufurahi, kuburudika na kucheza mziki wa bongo flava,” alisema Alikiba.

Utakumbuka kuwa ‘kolabo’ za Kimataifa za mwisho ambazo ziliwahi kufanywa na Alikiba zilikuwa ni mwaka 2021 kutoka kwenye album yake ya ‘Only One King’

Album hiyo yenye jumla ya nyimbo 16, ilibeba ‘kolabo’ za Kimataifa ambazo ziliwahusisha wasanii kama Mayorkum, Rudeboy, Nyashinski, Patoranking, Khaligraph Jones, Blaq Diamond, Sarkodie na Sauti Sol.

Hata hivyo, katika uzinduzi huo Alikiba aligusia pia kuhusu uwepo wake katika tuzo za Tanzania Music Award (TMA) na kusema kuwa ni kutokana na tuzo hizo kuheshimisha wasanii.

“Kitu ambacho kimepelekea yeye kuingia kwenye tuzo hizi za muziki nchini kwamba baada ya tuzo hizi kutuheshimisha kwa muda mrefu, ni watu ambao wanathamini mchango wetu, kwahiyo hichi walichokifanya leo kwa kurudisha tuzo inahamasisha wasanii kufanya kitu kizuri,” alisema Alikiba.

Mbali na heshima hizo, Alikiba aliongeza kwa kusema kuwa uwepo wa tuzo hizi pia umesaidia katika kuwajenga wasanii wa bongo fleva kutengeneza kazi ambazo zinakuwa na maadili yanayotakiwa katika jamii.

“Kwahiyo kitu kingine ni kwamba tuzo hizi pia zinawajenga wasanii kutengeneza nyimbo ambazo zinamaadili, nina uhakika pia TMA hawataweza kuingiza nyimbo ambazo hazina maadili, atleast kupitia hili kutakuwa na discipline kwa wasanii wetu,” aliongeza Alikiba.

Katika kipindi cha hivi karibuni pia, Alikiba amekuwa nyuma sana katika kuitangaza festival yake ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana katika kiwanda cha industry ya Bongo Flava.

Akitolea ufafanuzi hilo pia, Alikiba alisema kuwa sababu kubwa ambayo imefanya mashabiki zake waone kimya kuhusu upande wa festival ni kutokana na maswala ya media ambayo amekuwa akiyasimamia.

“Festival haijapotea ila tuliisitisha kutokana na haya mambo yanayoendelea ya media, tuliachana na unforgettable tukaanza kuface media, ndiomana hata ile ya unforgettable inaweza kuwepo hata kwenye media hii,” alisema Alikiba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags