Alikataa kuzaa kisa sikuwa na pesa, Sarkodie

Alikataa kuzaa kisa sikuwa na pesa, Sarkodie

Rapa kutokea Ghana Micheal Owusu Addo maarufu kama Sarkodie amemjibu Muigizaji Yvanne Nelson kupitia Diss Track (nyimbo) aliyoipa jina la “Try Me” baada ya mrembo huyo kudai kuwa alibeba ujauzito wa Rapa huyo lakini Sarkodie alimtaka atoe.

Yvonne aliyasema hayo kupitia kitabu chake “I am not Yvonne Nelson”. Sasa  ile kauli ya waswahili inayo sema dawa ya moto ni moto imetokea kwa Sarkodie kwa kumjibu mwanadada huyo kupitia wimbo aliouachia siku ya leo ambapo anasikika akisema.

“Sijawahi kutegemea kupitia haya, nilipanga nife nayo tu moyoni. Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuwa jasiri lakini huwezi kuchagua vitu vya kuongea?, jiheshimu” rapa  alisema maneno hayo.

Kwenye mistari mingine Sarkodie anasikika akisema “Mimi sikukwambia utoe ujauzito uliniambia una ujauzito, ndio ni kweli japo sikuwa tayari lakini nilikwambia usitoe ila wewe ulinieleza huwezi kubaki nao kwani ulitaka umalize kwanza masomo yako” Sarkodie.

Ukiacha mistari hiyo katika nyimbo yake kuna mengi Sarkodie ameyazungumza kuhusiana na sakata hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags