Alicia Keys akionesha tuzo zake

Alicia Keys akionesha tuzo zake

Mwanamuziki kutoka Marekani Alicia Keys, akionesha chumba maalumu ambacho ametunza tuzo zake mbalimbali alizopata kutokana na kazi yake ya muziki.

Keys alianza kujihusisha na kutunga nyimbo akiwa na umri wa miaka 12 na alisainiwa na lebo ya ‘Columbia Records’ akiwa na umri wa miaka 15.

Mpaka kufikia sasa Alicia Keys anaripotiwa kuwa na tuzo 16 za Grammy na kumfanya kuwa msanii wa nne wa kike kumiliki tuzo nyingi, pia ana tuzo tisa za Muziki za Billboard, nne za MTV VMA, tatu za MTV EMA, Tuzo 18 za NAACP na Tuzo 11 za Soul Train Music.

Keys amekuwa akitamba na ngoma zake kama ‘Girl on Fire’, ‘Try Sleeping with a Broken Hear’, ‘Karma’, ‘Superwoman’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags