Album ya Rich Mavoko yapigwa kalenda

Album ya Rich Mavoko yapigwa kalenda

Messi wa BongoFlava Rich Mavoko yupo tayari kuachia Album yake mpya ya fundi itayakotoka Machi 25 baada ya Machi 18 kama alivyotangaza awali.

Rich Mavoko anasema sababu ya kubadilisha tarehe ya kuachia Album hiyo ni kukumbuka historia ya mambo makubwa aliyoyofanya Hayati John Pombe Magufuli ambapo siku ya leo Machi 17 anatimiza mwaka mmoja wa kifo chake.

Taarifa ya Mavoko inaeleza kwamba "Album ya fundi ilitakiwa itoke kesho Tarehe 18 March lakini ni vyema zaidi kuchukua siku hizi kuyakumbuka yale makubwa na ya kihistoria yaliofanyika na mpendwa wetu Dkt John Pombe Magufuli"

"Aligusa maisha ya wengi na wengi bado tunamkumbuka. Hatuna budi kushukuru na kuendelea kumuombea amani popote alipo, Fundi itakufikia popote ulipo tarehe 25 March 2022,” ilieleza taarifa hiyo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags