Akutwa uchi kanisani, Njombe

Akutwa uchi kanisani, Njombe

Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana, lililopo Mtaa wa Matema, Halmashauri ya Mji wa Makambako, mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana.

Katibu wa Kanisa, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka kituo cha polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako, huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.

"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo ajisitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye vyombo vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia."

Aidha mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi, “Huyu mtu alisema alijikuta tu yupo madhabahuni tukamuuliza ulikuwa pekee yako akasema nilikuwa na mwenzangu," amesema Kisogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags