Aki atemana na mkewe, avuta jiko jipya

Aki atemana na mkewe, avuta jiko jipya

Mwigizaji wa Nigeria, Chinedu Ikedieze 'Aki', aliyejipatia umaarufu kupitia filamu ya 'Aki na Ukwa' amethibitisha kuachana na mkewe wa kwanza aliyemuoa mwaka 2011.

Aki na aliyekuwa mkewe Nneoma Nwaijah walifunga ndoa ya jadi tarehe 26 Novemba 2011 huko Obolo, Isiala Mbano, Jimbo la Imo.

Na kisha Desemba 9,2011 walifunga ndoa ya kikristo katika kanisa la Redeemed Christian Church of God - Parokia ya Abundant Grace lililopo Ogba, Lagos.

Katika harusi yao hiyo ilihudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wasanii kama Osita Iheme, maarufu kama Pawpaw, Uche Jombo, Rita Dominic, Mercy Johnson, Genevieve Nnaji, Monalisa Chinda, Susan Peters na wengine.

Licha ya hayo mwigizaji huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 46, ametangaza kuachana aliyekuwa mkewe na kuweka wazi kuwa sasa ameoa mwanamke mwingine aitwaye Stephanie Promise kwa ndoa ya siri, na hivi karibuni wamepata mtoto.

Kati ya filamu alizocheza mwigizaji huyo ni 'Aki na Ukwa', 'Aki and Pawpaw',Loyal Enemies Shedrack,Too Much Money,Two Sons of Ali,Village Rascals Aki,Terrible Twos na nyingine nyingi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags