Akataa kupooza, akimbia kilometa 10

Akataa kupooza, akimbia kilometa 10

Baada ya kupooza na kuambiwa hatoweza kutembea tena na madaktari mwanaridha Tim Marovt, aliwashangaza wengi baada ya kurudi tena kukimbia kwenye marathoni kwa kilometa 10 huku akiwa na magongo yake.

Akiwa likizoni katika visiwa vya Hawaii nchini Marekani, Marovt alipatwa na ‘surfer myelopathy’, jeraha la uti wa mgongo ambalo lilimsababishia kupooza, lakini kupitia juhudi kubwa na matibabu aliyopatiwa aliweza kuinuka tena na kuanza tena mbio za marathoni.

Marovt ali-share video hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alieleza kuwa mwaka 2024 anataka kufanya makubwa zaidi kwa kukimbia umbali mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags