Akanipandishia gauni ili nione vizuri…!

Akanipandishia gauni ili nione vizuri…!

Mkasa huu ulinipata Mwaka 1999, nakumbuka nilikuwa katika kuhangaika kutafuta kibarua, nilijikuta nikiwa kwenye ofisi moja ya jamaa yake kaka.

Nilifika hapo baada ya kaka yangu kuzungumza na huyo jamaa yale kuhusu ajira. Ilikuwa nikamwone ili kuona uwezekano wa kupewa ajira. Nilifika hapo ofisini kwa jamaa yake kaka kiasi cha saaa 2.15 asubuhi.

Nilipofika mapokezi, ambapo pia palikuwa panatumika kama ofisi ya watumishi wengine, nilikuta watu watano, wote wanawake. Mwanaume alikuwa mmoja, ambaye wakati naingia, naye alikuwa anatoka.

Nilisalimia na kumwambia katibu muhtasi shida yangu, ambapo aliniambia nikae kumsubiri bosi, ambaye kwa kawaida anafika pale ofisini saa tatu asubuhi au zaidi. Nilikaa kando kwenye makochi. mbele yangu kulikuwa na mwanamke ambaye alikuwa anafanya kazi zake.

 Alikuwa amekaa kihasara kwa kweli akiwa amevaa gauni fupi, alikuwa amaeachia mapaja yake wazi na niliweza hata kuona kule kunako utukufu bila wasiwasi. Nikiwa kijana shababi niliamua kufaidi sinema ile ya bure katika kupitisha muda kumsubiri bosi. Kwa hiyo nikawa napiga jicho kwenye mapaja yake ya haja maana mwanamke mwenyewe alikuwa ameumbika hasa. Nikiona yule dada ananitazama, navunja shingo na kujifanya simtazami yeye.

Niliendelea na sinema ile kama robo saa tu kabla yule dada hajaacha kufanya kazi yake. Alichukua kiti chake na kukitoa kutoka kwenye meza na kuja nacho karibu na makochi nilipokuwa nimekaa. Sikujua anafanya vile kwa sababu gani. Alipokiweka kiti kile pale mbele yangu, alipandisha gauni lake fupi hadi juu kabisa. 

Alipomaliza kufanya hivyo alikaa kitini huku akinitazama. Wale wanawake wengine pale ofisini waliacha kufanya kazi na kushikwa na mshangao. ‘Vipi mwenzetu, kuna nini kumekupata?’ Mmoja kati yao alimuuliza yule dada. ‘Nataka ayatazame mapaja na vingine kwa karibu ili afaidi sana. Naona anapata shida kuibaiba, haya tazama baba uridhishe nafsi yako.’

Kila mmoja alielewa maana yake, nikiwemo mimi. Ni kweli, nilikuwa ninamtazama kwa hila, lakini haina maana kwamba, nilikuwa namchungulia. Nilibaki nimeduwaa, nimepigwa na butwaa kubwa sana.

 Mmoja kati ya wale wanawake alisema, ‘dada Sia naye haishi vituko, hebu mwache kijana wa watu...’ mwingine alidakia, ‘utamuweza Sia na vituko vyake basi!’ yule mwanamke ambaye sasa nilijua anaitwa Sia alisema, ‘hapana, wanaume wengine bwana hawana adabu, macho wayuwayu sana. Nataka kiu yake iishe leo. Hebu cheki sasa uridhike.

Mlio wa gari la bosi wao ndiyo ambao uliniokoa kutoka katika kadhia ile. Aliposikia mlio huo wa gari, aliinua kiti chake na kurudi mezani pake huku akisema, ‘bahati yako, ungeniambia leo, nini kinang’aa zaidi, nyota au mbalamwezi.’

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags