Air Canada yaomba radhi kuwakalisha abiria kwenye viti vilivyo tapikiwa

Air Canada yaomba radhi kuwakalisha abiria kwenye viti vilivyo tapikiwa

Shirika la Ndege la Air Canada limeomba radhi baada ya kuwakalisha wateja wake wawili kwenye viti vilivyokuwa vimetapikiwa.

Inaelezwa kuwa baada ya wateja hao kukaa katika viti ambavyo vilikuwa vimefunikwa walianza kuhisi harufu mbaya na nguo zao kuanza kulowana sehemu walizokuwa wamekalia, ndipo waliamua kuita wahudumu wa ndege hiyo ili kupata msaada na walipotaka kufahamu ukweli walielezwa kuwa ulikuwa ni ubichi wa matapishi.

Hata hivyo wasafiri hao walivyojaribu kuomba kutafutiwa sehemu ya ziada ya kukaa wahudumu waliwajibu kuwa hakuna sehemu nyingine hivyo wavumilie, ndipo abiria hao walidai itakuwa ngumu kwa wao kukaa masaa matano katika viti vibichi.

Iliwabidi waombe ‘blankets’ kwa ajili ya kuweka kwenye viti. Hivyo basi baada ya tukio hilo taarifa zilianza kusambaa kwenye mtandao wa Facebook juu ya kilichotokea na ndipo shirika hilo la ndege limeamua kuchukua hatua ya kuomba msamaa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags