Ahmed Ally amuita Gamondi mazoezini

Ahmed Ally amuita Gamondi mazoezini

Msemaji wa ‘klabu’ ya #Simba, #AhmedAlly ametupa jiwe gizani baada ya kushusha ujumbe ambao baadhi ya mashabiki wametafsiri kuwa huwenda dongo hilo likawa linamlenga ‘kocha’ wa Yanga #MiguelGamondi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa #AhmedAlly ameandika ujumbe usemao

“Mwambieni mwalimu wenu aje na kwenye mazoezi yetu asiishie tu kwenye mechi”

Kufuatia ujumbe huo wadau wa mpira wa miguu wame-koment kuwa huwenda ujumbe huo ukawa unamlenga moja kwa moja ‘Kocha’ Gamondi baada ya kuonekana uwanjani akitizama ‘mechi’ za Simba.

#MiguelGamondi siku za hivi karibuni ameonekana katika ‘mechi’ mbalimbali moja wapo ikiwa ni ya ufunguzi wa #AFL ambapo ‘Timu’ ya Simba ilicheza na #AlAhly ya #Misri nyingine ikiwa ni #Simba na #Ihefu iliyotamatika kwa bao mbili kwa moja, ambapo Simba waliondoka na alama zote tatu.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags