Aguero kurejea timu ya taifa

Aguero kurejea timu ya taifa

Ebwana eeh!! unaambiwa mambo ni moto mambo ni fire hivyo ndivyo wanavyosema watoto wa mjini bwana sasa chukua taarifa hii hapa.

Nyota wa zamani wa timu ya Argentina Sergio Aguero amefanya mazungumzo na rais wa chama cha soka cha nchini humo AFA Claudio Tapia juu ya uwezekano wa yeye kuwemo kwenye benchi la ufundi la timu hiyo itakaposhiriki kwenye fainali za kombe la dunia mwezi november 2022 nchini Qatar.

Aguero mwenye umri wa miaka 33, ameichezea Argentina michezo 101 na kufunga magoli 41 huku akiitumikia kwenye michuano mitatu ya kombe la dunia (2010,2014 na 2018) sambamba na kutwaa kombe la Copa America mwaka 2021 alitangaza kustaafu soka kutokana na matatizo ya moyo akiwa na klabu yake ya Fc Barcelona

"Yalikuwa mazungumzo mazuri na Chiqui (Rais wa AFA),bado hatujajua nitakuwa kwenye nafasi gani lakini nitakuwepo na timu kwenye michezo ya kombe la dunia.Napenda kutumia muda mwingi na wachezaji maana nimetoka nao mbali sana na natamani kuwa karibu nao na kujaribu kutoa mchango wangu ili timu ya taifa ifanye vizuri zaidi" amesema Aguero.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags