Agoma kutoka nyumbani kwa Ex wake iliandelee kupata maokoto

Agoma kutoka nyumbani kwa Ex wake iliandelee kupata maokoto

Ebanaee!! Hivi mshawahi jiuliza kwanini wasanii wengi wa nje wanapigwa matukio sana na wapenzi wao wa zamani (Ex), basi bwana mwendo ni uleule jambo hili limemkuta tena muigizaji nguli wa filamu nchini Marekani, Kevin Costner mwenye umri wa miaka 68.

Ambapo ameiomba mahakama itumie nguvu kumtoa ex wake aliye fahamika kwa jina la Christine sehemu ambayo walio kuwa wanaishi pamoja kipindi ambacho bado walikuwa hawaja talikiana.

Ni baada ya mchakato wa talaka yao kuanza may mosi, ikiwa ni kwamujibu wa makubaliano ya Pre Nup walio saini pamoja.

Moja ya chombo cha habari nchini humo kimesema ex wa Kevin amegoma kutoka kwenye nyumba hio sababu anataka kutumia nafasi hiyo kupata pesa zaidi, tayari Kevin ameshampatia dola milioni 1.2 kama sehemu ya makubaliano yao na dola milioni 1.45 pala ambapo watatengana.

Pia atatoa dola 30,000 kila mwezi kwa matumizi ya watoto, dola 10000 kwaajili ya gharama za kuhama kwake, ila ex huyo bado anatengeneza mazingira ya kupata pesa  zaidi kutoka kwa mtalaka wake.

Sambamba na hayo mwanamke huyo alitakiwa kuondoka siku hiyo hiyo alipoomba talaka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags