Afunga ndoa na wanawake 30 kwa siku moja

Afunga ndoa na wanawake 30 kwa siku moja

Msanii wa muziki kutoka nchini #Nigeria, #Harrysong, amekuwa gumzo nchini humo baada ya kuvunja rekodi ya historia ya kuoa wanawake 30 ndani ya siku moja.

Harry amevunja rekodi hiyo ambayo mwanzoni ilikuwa ikishikiliwa na gwiji #FelaAnikulapo ambaye alioa wanawake 27 kwa siku moja nchini humo.

Nyota huyo wa Afrobeat ameonekana katika picha inayoonesha akiwa na idadi ya wanawake hao wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ambayo ni ishara ya kuwa wanawake hao ni maharusi wapya.

Msanii huyo aliwahi kuwa Msanii Bora wa Pop/R&B wa mwaka katika tuzo za Nigeria za 2014 baada ya kutolewa kwa wimbo wake ulioongoza chati ‘Beta Pikin’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags