Afariki kwa kupigwa teke tumboni

Afariki kwa kupigwa teke tumboni

Mmmmmm! Hii dunia inaenda wapi mana kila kukicha matukio ya ajabu yanazidi kuzuka tuu, Jovin Simon ambae ni ni mtoto wa miaka 10 Mkazi wa Mtaa wa Elimu Wilaya ya Geita amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na teke tumboni na Haruna Amini mwenye umri wa miaka 16.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo Ally Kitumbo amesema Jovin alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita huku akisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi kati  wawili hao.

"Huyu Mwanafunzi alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu na kiini cha tukio ni ugomvi, mwili  wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi wa Daktari” amesema Ally Kitumbo

Aidha Kaimu Kamanda amewataka  Wazazi wa mkoani humo  kuhakikisha wanawakanya Watoto wao kucheza michezo isiyokuwa na staha wawapo majumbani.

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags