Afariki baada ya kufanyiwa upasuaji mara 12

Afariki baada ya kufanyiwa upasuaji mara 12

Duh! Ifike mahali haya maswala ya upasuaji (surgeries) watu wayaweke kando na wakubaliane na jinsi walivyo basi bwana, muigizaji wa Canada Saint Von Colucci amefariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji mara 12 na kutumia zaidi ya Tsh Milioni 600 ili kufanana na msanii kutoka Korea wa kundi la BTS Jimin.

Saint amefia kwenye hospitali nchini Korea Kusini, alifanyiwa marekebisho mara 12 usoni ilikuweza kuigiza uhusika ya Jimin kwenye show mpya ya mtandaoni, marekebisho hayo ni ya Pua, kidevu, kuinua uso, kupunguza midomo, kuinua nyusi na kuinua macho.

Mwamba huyo alijua hatari zinazohusika na upasuaji huo ila alitaka sana kukamilisha muonekano huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags