Afariki akishindana kunywa pombe

Afariki akishindana kunywa pombe

Tukio hilo limetokea Sanyajuu Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro ambapo mtu mmoja aliye fahamika kwa jina la Ben amefariki dunia na wengine wanne wamelazwa baada ya kunywa pombe ya mashindano ambayo Mshindi wa kunywa chupa 8 za pombe kali atapewa shilingi elfu 50, mkate na sukari.

Akizungumza na repota kutoka Ayo Tv, Feliz Mrema ambae ni shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Dkt Shika alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kutoa ofa kwamba atakayemaliza chupa nne atapewa sukari kilo moja huku atakayemaliza chupa nane akiahidiwa kupewa sukari, mkate na shilingi elfu 50.

“Ben alivyokuja alikunywa na hakufikisha hata vinne palepale aliishiwa nguvu na kudondoka” alisema Shuhuda

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amesema tukio ni la kweli na kwamba mtu mmoja alifariki na wengine kukimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Chanzo Ayo Tv






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags