Aendelea kushikiria rekodi ya kuwa na nywele ndefu asili

Aendelea kushikiria rekodi ya kuwa na nywele ndefu asili

Mfanyabiashara kutoka New Orleans, Marekani, Aevin Dugas ameendela kushikilia rekodi ya kuwa na nywele ndefu za asili duniani ambapo mpaka kufikia sasa nywele hizo zina urefu wa 9.84 (25 cm).

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Guinness World Record’ Aevin aliingia kwenye kitabu ya Guinness mwaka 2010, nywele zake zikiwa na urefu wa 4 ft 4 (cm 132).

Hapo awali wakati anaingia katika kitabu hicho mwanadada huyo alieleza kuwa alitumia miaka 12 kukuza nywele hizo ambapo kwa sasa anatimiza miaka 24 toka aanze kufuga nywele hizo.

Aidha Aevin aliweka wazi kuwa huwa anapunguza ncha ya nywele hizo mara tatu kwa mwaka, na kutumia product tano wakati wa kuosha nywele.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post