Adidas yavunja mkataba na Beyonce

Adidas yavunja mkataba na Beyonce

Kampuni maarufu ya kutengezea nguo, viatu na vifaa mbalimbali ya Adidas imevunja mkataba wake na mwanamuziki mashuhuri kutoka nchini Marekani Beyonce, kutokana na mauzo ya bidhaa za mwanamuziki huyo kushuka.

Mkataba huo unavunjika ikisalia miezi 9 hadi umalizike, sababu zikitajwa kuwa ni kutofautiana katika masuala ya ubunifu kati yao na kushuka kwa mauzo ya bidhaa za 'Ivy Park' kutoka kwa Beyonce.  

Jarida la Wall Street limeripoti kuwa mauzo ya IvyPark yalishuka kwa zaidi ya 50%, ambapo ni Bilioni 93.6 mwaka 2022, kutoka makadirio ya mauzo ya bilioni 585. Mkataba huo ulikuwa ukimuingiza 'Queen Bey' Bilioni 46.8 kila mwaka.

Adidas inazidi kupata hasara mfululizo ikiwa ni miezi michache tangu kuvunjika mkataba kati yake na rapa Kanye West 'Ye', ambapo kampuni hiyo ilitangaza hasara ya trilioni 1.722 kutoka kwenye bidhaa za Yeezy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags