Adidas yamzawadia Messi pete za dhahabu

Adidas yamzawadia Messi pete za dhahabu

Mshambuliaji wa ‘Klabu’ ya Inter Miami kutoka nchini Marekani, Lionel Messi amezawadiwa pete nane za dhahabu na kampuni ya Adidas kuenzi matukio yake muhimu katika maisha ya ‘soka’.

Pete hizo ambazo alipewa na kampuni inayohusika na vifaa vya michezo duniani, Adidas zimeandikwa matukio yote makubwa na yamuhimu aliyowahi kuyapitia mchezaji huyo katika maisha yake ya ‘soka’.

Kati ya vitu vilivyoandika kwenye pete hiyo ni namba 91 ikiashiria ‘rekodi’ yake ya mabao aliyofunga mwaka 2012 na nyingine ikiwa ni nyota tatu ikimaanisha ushindi wake wa kombe la dunia kwa timu yake ya Taifa ya Argentina.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags