Adele atangaza kupumzika muziki

Adele atangaza kupumzika muziki

Mshindi wa Grammy mara 16 Adele ametangaza rasmi kupumzika kufanya shughuli za muziki kwa muda mrefu.

Hayo aliyasema Adele siku ya Jumamosi Agosti 31 wakati akiwa kwenye tamasha lake mjini Munich kwa kudai kuwa pindi atakapokamilisha makazi yake mjini Las Vegas Novemba, atachukua mapumziko ya muda marefu.

"Nimekuwa nikijitahidi kujenga maisha mapya kwa muda wa miaka saba iliyopita, na nataka kuyaishi. Nataka kuishi maisha mapya niliyoyajenga,"alisema Adele, huku sauti yake ikitetemeka

Aliongeza kuwa huenda asirudi jukwaani tena kwa muda mrefu. Hata hivyo bado anatarajia kuonekana jukwaani ifikapo Oktoba 25 hadi Novemba 23, kwenye onesho la mwisho la Las Vegas, Weekends with Adele.

Mbali na maisha ya muziki utakumbuka kuwa mwaka wa 2019, Adele na Simon Konecki ambaye wana mtoto mmoja pamoja walitangaza kuachana. Kisha mwaka 2021 akahusishwa kimapenzi na wakala wa michezo Rich Paul, hata hivyo uhusiano wao haujathibitishwa huku kukiwa na uvumi kuwa wanajiandaa kufunga ndoa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags