Adanganya kupata mshituko wa moyo, Akikwepa kulipa bili

Adanganya kupata mshituko wa moyo, Akikwepa kulipa bili

Mwanamume mmoja kutoka nchini Spain ambaye hajatambulika jina lake ameshikiliwa na polisi baada ya kudaiwa kudanganya kupatwa na mshituko wa moyo katika migahawa 20 ili kukwepa kulipa ‘bili’.

Mshukiwa huyo anadaiwa kufanya matukio hayo katika migahawa 20 kwenye eneo la Costa Blanca ambapo alinaswa katika mgahawa wa El Buen Comer, baada ya kuagiza chakula chenye thamani ya dola 37 ambazo ni zaidi ya tsh 90k, wadumu walipompeleka ‘bili’ alianza kufanya kama amepata mshituko wa moyo.

Ndipo ‘meneja’ wa mgahawa huo aliita gari la wagonjwa na polisi kwa ajili ya kutoa msaada ambapo baada ya polisi kufika waliweza kumtambua na kumshikilia kabla ya kupelekwa hospitali kwani kulikuwa tayari na taarifa zake za kukimbia kwenye migahawa mingine  Alicante.

Aidha Mwanamume huyo amewekwa kizuizini kwa siku 42 baada ya kukataa kulipa ‘faini’ huku wamiliki wa migahawa iliyotapeliwa wakipanga kuwasilisha malalamiko ya pamoja dhidi ya mwanaume huyo ambapo inaweza kusababisha kifungo cha miaka 2 jela.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags