Achomwa kisu kisa hajalipa pesa ya luku

Achomwa kisu kisa hajalipa pesa ya luku

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Blandina Fredi mkaazi wa kijiji cha Ilkrevi kata ya Olturoto, wilayani Arumeru mkoani Arusha anatuhumiwa kumuua Erick Adam ambaye ni msanii wa Bongo fleva na mfanyakazi wa kiwanda cha mikate kwa madai ya kudaiana pesa ya umeme (LUKU).  

Mashahidi wa tukio hilo wameeleza kuwa walishuhudia ugomvi ukiwa unaendela ambapo baadae walimkuta kijana huyo akiwa tayari ameshachomwa kisu na huyo mwanamke.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Mollel amethibitisha kifo hicho na kusema ni kweli kijana huyo amefariki na wamempeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa mkoani humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags