Achapwa viboko hadharani kwa kufumaniwa na mke wa mtu

Achapwa viboko hadharani kwa kufumaniwa na mke wa mtu

Mwanaume mmoja aliyefahamiaka kwa jina la Katayo Bote, Mkazi wa Kijiji cha Kibwera, mkoani Geita, amechapwa viboko hadharani pamoja na kulipishwa faini ya shilingi laki mbili baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.

Emmanuel Ndalawa ambaye ni mume wa mke aliyefumaniwa, amekiri kumfumania mwanaume huyo akiwa mtupu chumbani na mke wake, huku akisema hapo mwanzo mke wake alizidi kuonesha viashiria vya kuwa karibu na mtu huyo kadri siku zilivyozidi kwenda.

Mwanaume huyo ambaye ni mume wa wake wawili amesema amemfumania mke mdogo na Katayo katika chumba ambacho mke huyo amepangishiwa nyumbani kwa Katayo, akimaanisha aliyefumaniwa ni baba mwenye nyumba wao, anapoishi yeye na wake zake.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Simion Kisinza amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na uongozi wa kijiji umechukua hatua ya kuweka nidhamu kwenye eneo hilo kwa kumuadhibu Katayo Bote hadharani kutokana na kurudia kosa hilohilo kwa wapangaji wake kwa zaidi ya mara mbili.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post