Acha aibu, hizi ndizo fursa za kujikwamua kimaisha

Acha aibu, hizi ndizo fursa za kujikwamua kimaisha

Kama inavyofahamika kuwa suala la ajira, limekuwa janga la Taifa, asilimia kubwa ya wahitimu wamekuwa wakilia nalo.
Waswahili wanasema uoga wako ndiyo umasikini wako, na hili ni tatizo linalokumbwa baadhi ya vijana kutokana na kuhofia kujishughulisha na kazi ndogo ndogo kwa kuogopa kuchekwa.


Bila kuangalia watu watasema nini, leo nakuangazia kazi mbalimbali ambazo zinaweza kukukwamua kimaisha muhimu kuwa na mtaji tu na hapa ndiyo tunarudi kwenye suala la kujiajiri.
Kazi ni kazi kikubwa mkono uende kinywani, siku hizi hakuna anayechagua kazi, kwa hiyo fursa ninazozionesha hapo chini anaweza kufanya yeyote.

Usambazaji wa Magazeti
Licha ya mitandao ya jamii kuchukua nafasi kubwa katika utoaji wa taarifa, lakini bado watu wanapenda kusoma magazeti, hivyo bado kuna nafasi ya kazi kuyasambaza, unaweza kuifanya na kuhakikisha unatoka kimaisha ukiwa makini.

Zipo kampuni ambazo zinaajiri watu kwa ajili ya kupeleka magazeti majumbani yani hiyo ‘door to door’, wapo ambao wanasambaza kwa watu wanaouza rejareja na hata kupeleka mikoani so ni wewe kutoka magetoni na kufuata mpaka ofisi ilipo. Kutoka kwako ndiyo kupata kwako madili.

Maduka ya vyakula
Hapa kwanza ncheke, kuna fursa nyingine ziko wazi lakini watu kama hawazioni, kufanya biashara ya duka la chakula haitokufanya ulale njaa wala ukose faida kutokana kila iitwayo leo watu lazima watanunua kitu, kama sio unga basi mchele .


Ukiachilia mbali kuanzisha biashara hiyo pia unaweza kupata fursa ya kusambaza mahitaji kwa watu, siyo lazima kuwa na usafiri katika biashara hii kuna uwezekano wa kukodi gari kwa ajili ya kusambazia mizigo kwa wateja.

Life guard/ Bodyguard
Moja ya kazi ambayo inaenda kuheshimika zaidi kwa siku za usoni ni hii ya mlinzi binafsi, ambapo siku hizi hawa watu wanapata maokoto kutoka kwa wasanii kutokana na kuwasimamia kwenye ulinzi katika kazi zao mbalimbali.


Cha kufanya ni kwenda Gym kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuuweka mwili vizuri, na kupata mafunzo kutoka CPR pamoja na kuwatafuta watu ambao ni wazoefu kwa ajili ya kukufunza vitu mbalimbali ikiwemo utaratibu katika kazi.
Pia kazi ya ulinzi katika maofisi, najua hapa wengi wenu mnaweza kusema huyu dada anazungumzia nini, lakini ukipigika na maisha hata kazi unayoidengulia pia utaitamani na usiipate kwa wakati huo.

Job online
Siku hizi hakuna kitu kinachoweza kukupatia kipato kwa haraka zaidi kama mitandao ya kijamii, na ndiyo maana vijana wengi wanahangaika kutengeneza content kwa ajili ya mitandao mfano mzuri Tiktok, watu wengi wamekuwa wakipata madili ya matangazo kutokana na mtandao huo.

So wewe kama kijana unaweza kutumia kipaji ulichonacho na hilo bando unaloweka kwa ajili ya kuposti memes, ni vyema kufanya chochote ambacho kinaweza kukupa mwangaza wa kujikimu kimaisha.

Tumia mitandao kama YouTube kutengeneza content, inaweza kukusaidia kuona fursa zilizo mbele yako. Angalia wachekeshaji, waigizaji na hata waimbaji wanatumia mitandao kuendesha maisha yao.

Duka la vinywaji
Mchongo mzima uko hivi, hii biashara ili uweza kuiona utamu wake ifanye katika sehemu yenye mzunguko wa watu , mfano Magufuli stand, Kariakoo, Buguruni, Kigamboni Feri na sehemu ambazo zinamkusanyiko wa watu.
Nimezungumzia fursa hii katika maeneo hayo kuwa na mzunguko mkubwa watu, hivyo ni lazima baadhi yao watatumia vinywaji acha kukaa kizembe chukua hiyooo.

Biashara ya kuuza chakula
Siku za hivi karibuni watoto wa kiume wamezinduka na kujikita katika biashara mbalimbali za Mama Ntilie. Kama kupika kila mtu anajua cha kuzingatia ni kuongeza ujuzi, wakinamama wengi wanauza chakula mchana lakini vijana wanauza usiku so wewe unaangalia sehemu ambayo inamzunguko mkubwa wa watu usiangalie wanapika watu wangapi unachotakiwa ni kuboresha chakula chako ili uwavutie wateja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags