Aachiwa huru baada ya kukaa gerezani  miaka 28

Aachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 28

Mwanaume mmoja nchini Marekani aliefahamika kwa jina la Lamar Johnson mwenye umri wa miaka 50 alikaa gerezani kwa takriban miaka 28 kwa mauaji ambayo amekuwa akikana kutenda imethibitishwa kuwa hana hatia katika hukumu iliofanyika huko Missouri.

Alitoka nje ya chumba cha mahakama ya St Louis akiwa mtu huru baada ya uamuzi wa Jaji David Mason siku ya Jumanne.Hakimu alisema alitoa hukumu hiyo baada ya mashahidi wawili kutoa ushahidi wa wazi na wa kuridhisha" kwamba  Johnson hakuwa na hatia.

Johnson alipatikana na hatia ya kumuua Marcus Boyd mwaka 1994. “Ninashangazwa na hilo mno” alisema  baada ya kutoka nje ya chumba cha mahakama.

Mwaka jana, Wakili Kim Gardner alikuwa amewasilisha ombi la kutaka mtuhumiwa huyo aachiliwe huru baada ya kufanya uchunguzi pamoja na shirika lisilo la kiserikali la Innocence Project.

Kufuatia kusikilizwa kwa kesi hiyo Jumanne, timu ya wanasheria ya Lamar Johnson ilikosoa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ambayo ilishinikiza kumweka gerezani.

Aidha ofisi hiyo haikuacha kudai Lamar alikuwa na hatia na ilikuwa vyema kumfanya ateseke na kufa gerezani mawakili wa Johnson walisema katika taarifa.

Msemaji wa mwanasheria mkuu alisema katika barua pepe kwamba ofisi hiyo haitachukua hatua zaidi katika kesi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags