50 Cent amshangaa Nick kuwa na watoto 12, Hataki majukumu

50 Cent amshangaa Nick kuwa na watoto 12, Hataki majukumu

Rapper mkongwe wa Marekani 5O Cent ameweka wazi kuwa haiwezi kutokea akawa na watoto wengi kama ilivyo kwa muigizaji, mchekeshaji na mtangazaji Nick Cannon ambaye hadi sasa ana watoto 12.

50 Cent amefunguka hayo wakati wa mahojiano yake na Brian J. Roberts wa Forbes, na kudai kuwa anamshangaa sana Nick kwa kuwa na watoto wengi kutoka kwa wanawake tofauti tofauti.

Huku kwa upande wake 50 Cent sababu kubwa ya kutokuwa na watoto wengi amedai kuwa hataki majukumu kwa wanawake tofauti tofauti atakao wazalisha.

Imekuwa  kawaida kwa 50 Cent na Nick kutupiana Maneno mara kwa mara, kwani kabla ya 50 kuzungumza hayo Nick akiwa kwenye podcast yake ya “The Daily Cannon”, alimtupia maneno 50  kuhusiana na mwili wake kwa kudai kuwa ni mnene kiasi kwamba shingo yake nyuma ina nyama kama ameweke kifurushi.

Hadi sasa 5O Cent anamtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 26 anayefahamika kama Marquise Jackson's.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags