50 Cent alinunua viti 200 kwenye show ya Ja rule na kuviacha wazi

50 Cent alinunua viti 200 kwenye show ya Ja rule na kuviacha wazi

Upinzani umekuwa kitu cha kawaida kwa watu wanaofanya jambo la kufanana, kama ilivyo kwa wafanyabiashara katika kuvuta wateja, kwenye michezo kama ilivyo simba na Yanga, lakini japo hilo linaonekana hata katika upande wa muziki pia lipo.

Na ndiyo maana unaweza kukuta msanii fulani akawa na upinzani na mwingine kwenye upande wa  kazi zao kwa kila mmoja kutaka mashabiki wamuone ndiye bora. Jambo hilo si tu Tanzania bali Duniani kote upinzani unatokea.

Tujikumbushe tukio la wapinzani wawili wa muziki wa #HipHop kutoka nchini Marekani, 50 Cent na Ja Rule, ambao kutokana na upinzani wao mwaka 2018 ikapelekea 50 Cent kununua ‘tiketi’ 200 za viti vya mbele kwenye tamasha la Ja Rule, na kuviacha wazi kwa lengo la kumkomoa Ja Rule ili aonekane hajajaza watu kwenye tamasha hilo.

Kutokana na tukio hilo ilipelekea viti vyote vya mbele kuachwa wazi huku mashabiki waliokuwa wamebahatika kupata ‘tiketi’ wanakadiriwa kuwa hawakufika hata 50 wakiwa wamekaa viti vya nyuma kabisa mbali na sehemu anayo tumbwiza Ja Rule .

Ugomvi wa wakali hawa wawili unatajwa kuwa wa kitambo kwani ulianza mwishini mwa miaka ya 90, na kila mmoja amekuwa akimvimbia mwenzake kwa namna yake hadi kufikia 50 Cent kunuua tiketi hizo 200 za viti vya mbele katika tamasha la Ja Rule na Ashanti, ambapo kila kiti kilikuwa kikiuzwa kwa dola 15 ambayo  ni zaidi ya Tsh 30 elfu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags