27 wafariki katika mgodi wa dhahabu, Peru

27 wafariki katika mgodi wa dhahabu, Peru

Watu 27 wamefariki katika ajali ya mgodi wa dhahabu nchini Peru, katika ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita.

Kampuni ya mgodi ya Yanaquihua, ilisema wachimba migodi 175 waliokolewa. Maafisa walisema wachimbaji hao walikuwa wakifanya kazi takriban mita 100 (futi 330) chini ya ardhi wakati moto huo ulipozuka.

Picha za vyombo vya habari vya ndani zilionyesha moto na moshi ukifuka kutoka kwenye kilima.

Aidha kulingana na tovuti ya habari ya Peru (rpp.pe), moto huo ulichochewa na viunga vya handaki vya mbao vya mgodi wa dhahabu wa La Esperanza, wengi wao wakiwa wamelowa mafuta.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags