2025 Kufanya Kazi Mwisho Alhamisi

2025 Kufanya Kazi Mwisho Alhamisi

Serikali ya Tokyo nchini Japan inampango wa kuweka ratiba mpya ya kazi ifikapo mwaka 2025 ambapo wafanyakazi wote wa serikalini wataingia kazini siku nne tu ndani ya wiki huku siku za mapumziko zikiwa tatu ambazo ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Wakati akiwa kwenye kikao cha Bunge Gavana wa jiji hilo Yuriko Koike ameweka wazi kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia Aprili 2025 huku lengo kuu la kufanya hivyo likitajwa kuwa ni wafanyakazi kupata muda zaidi na familia zao.

Utakumbuka kuwa Oktoba 2024 Japan ilitangaza kupunguza wiki ya kazi kuwa siku nne kwa wafanyakazi wote wa serikalini ifikapo mwaka wa fedha 2026.

Aidha mbali na kupunguza siku hizo lakini pia moja ya sababu kubwa ya kupunguza siku za kufanyakazi ni kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na changamoto ya kiwango cha uzazi kuwa mdogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags