162 wafutiwa shahada zao

162 wafutiwa shahada zao

Chuo Kikuu cha St. Augustine kimebatilisha Shahada ilizotoa kwa madaktari wa afya 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St. Francis (SFUCHAS), kuanzia mwaka 2015-2019.

Taarifa kutoka chuoni hapo zinadai madaktari hao wamegoma kurejesha nyaraka za matokeo (Transcripts) ambazo walipewa bila baraza la seneti la chuo kuwa na taarifa na kuziidhinisha.

Aidha taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa Seneti ya Chuo, Balozi Prof. Costa Mahalu, imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mkutano wa Seneti, uliofanyika Februari 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags