12 wafariki dunia baada ya uwanja kuporomoka.

12 wafariki dunia baada ya uwanja kuporomoka.

Takribani watu 12 wamefariki dunia nchini El Salvador baada ya uwanja wa michezo wa Cuscatlan kuporomoka.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mechi ya Alianza na Santa Ana ya Fas siku ya Jumamosi, Mei 20 maafisa wa nchi hiyo wamehusisha tukio hilo na kuuzwa kwa tiketi kupita kiasi na utoaji wa tiketi za udanganyifu.

Aidha Rais Nayib Bukele alielezea tukio hilo kama ambalo halijawahi kutokea na kwamba kila mtu atachunguzwa amesema.

“Kila mtu atachunguzwa zikiwemo timu, mameneja, viongozi wa viwanja, ligi na shirikisho”alisema Buleke

Sambamba na maafisa pia walisema kuwa watu 90 walikuwa wakipokea matibabu, na kwamba wanaume, wanawake na watoto walio pata majeraha makubwa walipatiwa matibabu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags